Bunge la Afrika Kusini lapitisha pendekezo la kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel
2023-11-22 10:14:39| cri

Bunge la Afrika Kusini limepitisha pendekezo la kusitisha kwa muda uhusiano wa kidiplomasia na Israel na kufunga ubalozi wa Israel nchini humo hadi Israel itakapokubali kusitisha mapigano na kushiriki kwenye mazungumzo yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa.

Tangazo lililotolewa na bunge hilo baadaye limesema japo pendekezo hilo halishurutishi serikali kisheria, lakini spika wa bunge ana jukumu la kuomba Rais na mamlaka husika za serikali kulizingatia. Waziri katika ofisi ya rais wa Afrika Kusini Bw.Khumbudzo Ntshavheni alisema tarehe 20 kuwa baraza la mawaziri bado halijatoa uamuzi kama litafunga ubalozi wa Israel nchini humo.