Jamhuri ya Kongo yatangaza Novemba 22 kuwa Siku ya Taifa ya Maombolezo kwa kumbukumbu ya wahanga wa mkanyagano
2023-11-22 10:14:11| cri

Tukio la mkanyagano lilitokea huko mji wa Brazzaville nchini Jamhuri ya Kongo usiku wa tarehe 20 hadi alfajiri wa tarehe 21 mwezi huu na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 37.

Waziri mkuu wa nchi hiyo Anatole Collinet Makosso ameenda hospitalini kuwatembelea majeruhi na kuunda kikosi kazi cha serikali cha kushughulikia tukio hilo, ambacho kimeamua kuweka tarehe 22 Novemba kuwa Siku ya Taifa ya Maombolezo. Bendera zinapeperushwa nusu mlingoti na baa, kumbi za dansi na kumbi zingine za burudani zimefungwa. Timu ya pamoja ya uchunguzi itaundwa kutafuta chanzo cha ajali hiyo.