Rwanda yaorodheshwa ya tano kwa uendelevu wa mazingira
2023-11-22 23:11:42| cri

Ripoti mpya kuhusu uendelevu wa mazingira inaonesha kuwa juhudi katika mikakati endelevu, programu, na uwekezaji zimeifanya Rwanda kuwa nchi ya tano kwa uendelevu wa mazingira barani Afrika.

Licha ya changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi zinazoathiri zaidi nchi zinazoendelea, Rwanda imepiga hatua za kuhimiza juhudi kwa lengo la kuharakisha ukuaji wa uchumi unaoongozwa na sekta binafsi na kuongeza tija.

Hatua za kimazingira zilizopigwa na bara la Afrika zinaangazia ukweli kwamba nchi nyingi za Mashariki ya Kati na Afrika zimeongeza juhudi katika mbinu endelevu.

Kadi ya alama inachambua nchi 17 ikizingatia viashirio sita muhimu vikiwemo uwekezaji na teknolojia ya kijani, miundombinu endelevu na usafiri, utawala bora na utoaji taarifa, mpito wa nishati, mifumo ikolojia ya mazingira na mzunguko. Rwanda imeshika nafasi ya tano kwenye orodha iliyoongoza kwa Afrika Kusini, Falme za Kiarabu, Misri na Saudi Arabia, ikifuatiwa na Kenya, Uganda, Ghana, Morocco, Qatar, Tanzania, Nigeria, Bahrain, Kuwait, Cote d'Ivoire, Oman, na Msumbiji.