Watu zaidi ya 37 wafariki katika tukio la kukanyagana nchini Jamhuri ya Kongo
2023-11-22 08:38:41| cri


 

Serikali ya Jamhuri ya Kongo jana imesema, watu zaidi ya 37 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika tukio la kukanyagana lilitokea usiku wa tarehe 20 huko Brazzaville, mji mkuu wa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na serikali imesema, tukio hilo lilitokea kwenye uwanja wa michezo ambapo zoezi la kuajiri askari wapya lilikuwa linafanyika.

Serikali ya Jamhuri ya Kongo imeunda kikundi cha dharura kushughulikia tukio hilo.