Umoja wa mataifa kusaidia wanawake wa Tanzania kujengewa uwezo masomo ya sayansi
2023-11-22 10:12:50| cri

Shirika linaloshughulikia mambo ya wanawake la Umoja wa Mataifa (UN Women) kwa kushirikiana na kampuni binafsi nchini Tanzania wamesaini makubaliano ya kusaidia wasichana na wanawake wa vijijini na mijini kujifunza masomo ya sayansi.

Shirila hilo linaoanza kuongeza nguvu kwenye programu ya 'Code like a Girl' inayohamasisha kujifunza masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi, hisabati na stadi za uandishi wa kidijitali, ikiwa imelenga kutoa mafunzo hayo kwa wanawake na wasichana wenye umri wa miaka 17 hadi 25 ili waweze kusoma taaluma hiyo.

Mwakilishi wa UN Women Tanzania, Hodan Addou amesisitiza umuhimu wa kuwajumuisha wasichana katika sekta ya Tehama kama jambo la lazima, ili kuongeza uwakilishi wa wanawake katika nyanja hizo, amesema wanawake wanaposhiriki katika Tehama, huleta mitazamo tofauti ambayo ni muhimu kwa uvumbuzi na matokeo bora.