EAC yachukua hatua kukabiliana na suala la wakimbizi katika kanda hiyo
2023-11-22 08:41:29| CRI

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imesema kuwa bado inashirikiana na wenzi wake katika kutunga sera na miongozo unayolenga kukabiliana na ukiukaji wa haki za binadamu na changamoto zinazowakabili wakimbizi katika kanda ya Afrika Mashariki.

Ahadi hiyo ilitolewa na kaimu katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Andrea Aguer Ariik Malueth, anayeshughulika na miundombinu, uzalishaji, na sekta za jamii na siasa wakati alipofanya ziara katika makao makuu ya Jumuiya hiyo mjini Arusha, Tanzania. Malueth ameeleza juhudi za Jumuiya hiyo katika kukabiliana na hali tete, kuanzisha na kusimamia mfumo wa amani wa kikanda, utekelezaji wa mchakato wa kidemokrasia wa uchaguzi, kuboresha upatanishi wa kikanda na wa pande mbili na mchakato wa maafikiano, na kuunga mkono mpito wa kisheria katika kanda hiyo.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa kanda ya Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika, na Maziwa Makuu, Mamadou Dian Balde, amesema kuna haja ya kuwawezesha wakimbizi na ujuzi wa maisha kupitia mafunzo, na kuhakikisha kuwa wanakuwa na maisha mazuri.