Bunge la Afrika Kusini lapitisha muswada wa kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel
2023-11-22 08:37:18| cri

Bunge la Afrika Kusini jumanne limepitisha muswada wa kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel kufuatia matokeo ya kura zilizopigwa na wabunge, ambapo kura 248 ziliunga mkono muswada huo na kura 91 ziliupinga.

Baada ya kupitisha muswada huo, Bunge hilo lilisema, muswada huo hauingilii serikali kisheria, lakini Spika ana jukumu la kuwasilisha muswada huo kwa rais na idara husika za serikali.

Hata hivyo, jumatatu wiki hii, Baraza la Mawaziri la Afrika Kusini lilitangaza kuwa bado halijaamua iwapo litafunga Ubalozi wa Israel nchini Afrika Kusini.