Kampuni ya Huawei yazindua mradi wa “Mbegu za Baadaye” nchini Botswana
2023-11-22 08:40:14| CRI

Kampuni ya teknolojia na mawasiliano ya China, Huawei, imezindua mradi wa “Mbegu za Baadaye” nchini Botswana jana jumanne, ikilenga kuibua vipaji vya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) na viongozi vijana kwa ajili ya siku za baadaye, na kuboresha maendeleo ya jamii za kidijitali.

Wanafunzi 25 wa vyuo vikuu nchini Botswana watashiriki moja kwa moja kwenye mradi huo kuanzia leo hadi Novemba 27.

Akizindua mradi huo mjini Gaborone, Meneja mkuu wa kampuni ya Huawei tawi la Botswana, David Zhang amesema, wanafunzi hao watapata uzoefu mkubwa, ikiwemo mihadhara ya kiufundi, semina za uongozi, utamaduni wa China na mawasiliano na vijana wengine kutoka nchi mbalimbali duniani.