Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa kufanya ziara nchini China
2023-11-23 14:37:35| cri

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi Mao Ning amesema, kutokana na mwaliko wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi, waziri wa Ulaya na mambo ya nje wa Ufaransa Bi Catherine Colonna atafanya ziara nchini China Novemba 23 na 24 na kuhudhuria kikao cha sita cha utaratibu wa mawasiliano ya ngazi ya juu ya kiutamaduni kati ya China na Ufaransa.