Marais wa China na Uruguay wafanya mazungumzo
2023-11-23 08:42:11| CRI

Rais wa China Xi Jinping jana katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, amefanya mazungumzo na rais wa Uruguay Luis Lacalle Pou ambaye yupo ziarani nchini China.

Marais hao wametangaza kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili utapandishwa na kufikia ngazi ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote.

Katika mazungumzo hayo, rais Xi amesema China inapenda kushirikiana na Uruguay kuboresha uhusiano wa pande mbili, na kupanua ushirikiano ili kuchangia zaidi maendeleo ya nchi hizo mbili na kunufaisha zaidi wananchi wao.

Kwa upande wake rais Luis Lacalle Pou amesema Uruguay inapenda kuonesha umuhimu katika kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya Amerika Kusini na ujenzi wa Baraza la Jumuiya ya China na Amerika Kusini na nchi za Caribbean.