Usitishaji vita huko Gaza kuanza Alhamisi asubuhi
2023-11-23 08:42:02| cri

Afisa mkuu wa kundi la Hamas Bw. Moussa Abu Marzouk, amesema, makubaliano ya kusitisha vita katika Ukanda wa Gaza yataanza leo Alhamisi saa nne asubuhi kwa saa za huko, na mateka 50 wataachiliwa, wengi wao wakiwa ni raia wa kigeni.

Habari zinasema, Israel na kundi la Hamas Jumatano zilithibitisha kukubali pendekezo la kusitisha mapigano chini ya upatanishi wa Qatar.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel imesema, chini ya makubaliano hayo, watu 50 waliotekwa nyara, wengi wakiwa ni watoto na wanawake, wataachiwa huru, huku wafungwa 150 wa Palestina wakiwemo wanawake na vijana wataachiwa kutoka jela nchini Israel.