Polisi wa Uganda wateketeza dawa haramu za Shs3b zilizokamatwa kwa wasafiri katika uwanja wa ndege wa Entebbe
2023-11-23 14:14:13| cri

Polisi katika eneo la mji wa Kampala wamechoma zaidi ya kilo 56 za dawa za kulevya zenye thamani ya Sh3 bilioni za Uganda zilizokamatwa kwa abiria waliokuwa wanasafiri kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe kati ya 2020 na 2023, uchomaji wa dawa hizo ulifanyika katika eneo la Polisi la Nsambya.

Mkurugenzi wa uchunguzi katika polisi wa shirika la ndege la Civil Aviation Bi Juliet Baguma amesema dawa hizo huvuruga akili ya watumiaji na kuwafanya wajihusishe na makosa kama vile ubakaji, mauaji, wizi na ugaidi.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi ya mwaka wa 2022 ya uhalifu, matukio ya dawa za kulevya yaliongezeka maradufu hadi kufikia 2,797 ikilinganishwa na 1, 668 yaliyoripotiwa mwaka 2021.

Ripoti hiyo hiyo inaonyesha kuwa jumla ya washukiwa 4, 818 walikamatwa na kushtakiwa mahakamani, wakiwemo watoto 137.