Mtafiti kutoka Tanzania nchini China ashinda tuzo ya kimataifa ya mwanasayansi hodari
2023-11-23 10:10:09| cri

Mwanafunzi kutoka Tanzania anayepata mafunzo yake nchini China Dk. Manala Mbumba, ametunukiwa tuzo ya mwanasayansi hodari wa kimataifa. Dr. Mbumba ni mwanafunzi aliyesomea shahada ya uzamivu ya nishati mbadala na nishati safi kutoka Chuo Kikuu cha Umeme cha Kaskazini cha China nchini China.

Kwa sasa amejikita kwenye utafiti wa utulivu wa joto wa kwenye vifaa maalum vya paneli za nishati ya jua. Kabla ya kuhamia China, Dr. Manala alikuwa akifanya kazi kama mhadhiri msaidizi na mshauri wa muda wa miradi ya nishati mbadala katika Taasisi ya Kitaifa ya Usafirishaji (NIT).

Tuzo za Kimataifa za Wanasayansi Maarufu ni tuzo ambazo hutolewa kwa watu binafsi au timu kwa michango yao bora kwenye eneo maalum la utafiti.

Tuzo hizi zinatambua ubora katika utafiti asili, fikra bunifu, na ubora na athari za kazi iliyochapishwa.