Ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na Afrika ni wa kunufaishana
2023-11-23 14:42:25| CRI

“Ripoti ya Mwaka 2023 ya Uwekezaji wa Kampuni za China barani Afrika” imetolewa hivi karibuni. Katika miaka ya hivi karibuni, uwekezaji wa China barani Afrika umeongezeka kwa mfululizo, na mafanikio ya ushirikiano wa uwekezaji kati ya pande hizo mbili yamezidi kudhihirika.

Ripoti hiyo imechambua uwekezaji wa China barani Afrika kupitia miradi 21 ikiwemo Kituo cha Majaribio ya Kilimo cha Mpunga cha Madagascar, Jukwaa la Biashara ya Mtandaoni Kilimall, na Reli ya Nairobi-Malaba, na kudhihirisha kwamba ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na Afrika umenufaisha pande hizo mbili, na kupata mafanikio makubwa.

Katika miaka ya hivi karibuni, uwekezaji wa China barani Afrika umeongezeka mwaka hadi mwaka. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2022, uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika umezidi dola bilioni 47 za Kimarekani, na zaidi ya kampuni 3,000 za China zimewekeza na kuanzisha biashara barani Afrika. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika ulizidi dola bilioni 1.82 za Kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 4.4 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki. Kwa mujibu wa Mkutano wa Dakar wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, hadi ifikapo mwaka 2035, uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika utafikia dola bilioni 90 za Kimarekani, na kutarajiwa kushika nafasi ya kwanza duniani.

Afrika ni bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea duniani, inahitaji uwekezaji wa kigeni ili kuboresha miundombinu iliyo nyuma, kuinua kiwango cha ukuaji wa viwanda, kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kutokomeza umaskini, na kuhakikisha usalama wa chakula. Ikiwa mwenzi wa kuaminika wa Afrika, China imefanya uwekezaji mkubwa barani Afrika. Kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, China imewekeza na kujenga miradi mikubwa barani Afrika, ikiwemo zaidi ya kilomita 6,000 za reli, zaidi ya kilomita 6,000 za barabara, karibu bandari 20, zaidi ya vituo 80 vya umeme, maeneo 25 ya kiviwanda, na zaidi ya vituo 500 vya majaribio ya kilimo. Zaidi ya hayo, miradi mingine ya kawaida ya uwekezaji kati ya China na Afrika haihesabiki, ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo endelevu ya uchumi wa nchi za Afrika. Mbali na fedha, China pia inatoa teknolojia ya juu kwa Afrika. Rasilimali hizi zimehimiza sana ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika. Aidha, uwekezaji wa China barani Afrika pia umeleta nafasi nyingi za ajira kwa watu wa Afrika.

Ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na Afrika pia una umuhimu mkubwa kwa China. kupitia ushirikiano huo, China inaweza kuhamisha uwezo wa uzalishaji ambao ni mkubwa zaidi kuliko mahitaji ya ndani, kuboresha mnyororo wa uzalishaji duniani, kuhakikisha usalama wa maliasili, na kuendeleza kampuni zake.