Habari kutoka mamlaka ya usalama ya Cameroon inasema jana tarehe 22 kuwa kundi la itikadi kali la Boko Haram lilishambulia maeneo mawili ya makazi Kaskazini ya Mbali na kusababisha vifo vya raia wasiopungua watatu. Tangu mwezi Novemba, wapiganaji wa kundi hilo wamewaua raia takriban 12 na askari wawili.
Habari zinasema nchi hiyo imeimarisha hatua za usalama katika eneo hilo wakati shughuli za kusherehekea mwisho wa mwaka zikikaribia na katika wiki mbili zilizopita, wapiganaji wasiopungua 10 wameuawa na wengine kadhaa wamekamatwa.