Mazungumzo ya amani ya Ethiopia yamalizika bila kufikia makubaliano
2023-11-23 08:45:11| CRI

Mshauri wa Waziri Mkuu wa Ethiopia kuhusu masuala ya usalama wa ndani, Redwan Hussein amesema, mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Ethiopia na kundi la waasi la Ukombozi la Oromo (OLA) yamemalizika bila kufikia makubaliano.

Kupitia mtandao wa kijamii wa X, Bw. Hussein amesema mtazamo usio sahihi na masharti yasiyowezekana ya wajumbe wa OLA ni sababu kuu ya kushindwa kufikia makubaliano hayo.

Mwezi April, wajumbe wa pande hizo mbili walikutana kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kwa ajili ya mazungumzo ya makubaliano ya amani, lakini hawakufikia makubaliano.

Mwezi Mei, 2021, bunge la Ethiopia lilipiga kura na kulitangaza kundi la OLA kuwa la kigaidi, uamuzi ambao umedumu mpaka sasa.