Waziri Mkuu wa China ahutubia mkutano wa kilele wa Kundi la Nchi 20 uliofanyika kwa njia ya video
2023-11-23 08:42:27| cri


 

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang jana usiku ameshiriki kwenye mkutano wa kilele wa Kundi la Nchi 20 (G20) uliofanyika kwa njia ya video.

Katika hotuba yake, Bw. Li Qiang amesema bado kuna matatizo mengi kwenye njia ya kufufuka kwa uchumi wa dunia, na kama rais wa China Xi Jinping alivyosema, nchi wanachama wa G20 wanapaswa kubeba wajibu wa nchi kubwa na kuonesha umuhimu wa mfano mzuri. Bw. Li amelitaka Kundi hilo kuendelea kutoa kipaumbele katika maendeleo, kutilia maanani ushirikiano wa maendeleo, kuharakisha utimizaji wa ongezeko la uchumi wa dunia linaloshirikisha pande zote, na kupinga kulifanya suala la maendeleo liwe wa kisiasa na kisalama.

Bw. Li amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ufufuaji wa uchumi na ustawi wa dunia.