WHO: Asilimia 65 ya watu wa Sudan wakosa huduma za afya kutokana na mapigano
2023-11-23 10:13:35| cri

Shirika la Afya Duniani (WHO) tarehe 22 limesema mapigano nchini Sudan yameleta uharibifu mkubwa kwa mfumo wa afya wa nchi hiyo, ambapo asilimia 70 ya taasisi za matibabu zimesitisha huduma zao na asilimia 65 ya watu wake wanakosa huduma ya afya huku wafanyakazi wengi wa afya hawajapewa mishahara kwa miezi saba. Licha ya hayo, maambukizi ya magonjwa mengi kama vile kipindupindu, homa ya dengue, surua yamelipuka katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo na mamilioni ya watu wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa.