Kampuni ya software ya China yasaini makubaliano na Kenya kuongeza ushirikiano wa kiteknolojia
2023-11-23 08:44:36| CRI

Kampuni ya Supermap International ya China imesaini makubaliano na Kurugenzi ya Utafiti wa Rasilimali na Utambulisho wa Mbali ya Kenya (DRSRS) yanayolenga kuboresha ufanisi wa teknolojia ya utambuzi sahihi wa maeneo ya kijiografia.

Mkurugenzi wa DRSRS Moses Akali amesema, makubaliano hayo yanahusisha mafunzo kwa zaidi ya maofisa 70 wa Kenya, wasomi na watu binafsi katika mifumo ya juu ya Taarifa za Kijiografia (GIS) katika kipindi cha mwaka mmoja. Amesema kwa kutumia teknolojia za GIS, Supermap itaiwezesha Kenya kutumia vizuri data za kijiografia, ambazo zitajumuisha maeneo mengi ikiwemo usalama wa chakula, usimamizi wa majanga ya asili, mabadiliko ya tabianchi na udhibiti wa utoaji wa hewa chafu.