China na Marekani zimefikia makubaliano kuhusu suala la mabadiliko ya tabianchi, na kuleta msukumo mpya katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na changamoto hiyo.
Baada ya duru mbili za mazungumzo, China na Marekani huko California zimetoa taarifa ya pamoja ya kuhusu kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, pande hizo mbili zimekubaliana katika mambo mbalimbali yakiwemo mabadiliko ya matumizi ya nishati, utoaji wa hewa zinazoweza kuongezeka joto licha ya hewa ya kaboni, na uratibu wa kupunguza utoaji wa hewa za kuongeza joto na uchafuzi kwa hewa. Zaidi ya hayo, pande hizo mbili pia zimeamua kuanzisha kikundi cha kazi cha kuimarisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuanzia mwaka 2020 hadi 2029. Taarifa hiyo yenye vipengele 25 inasisitiza kwamba, China na Marekani zitatekeleza vyema Makubaliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na Makubaliano ya Paris. Katika mkutano kati ya Marais wa nchi hizo mbili uliofanyika siku iliyofuata, pande zote mbili zimesisitiza kwa kauli moja kwamba China na Marekani zinapaswa kuharakisha juhudi za kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi, na kuhimiza kwa pamoja mafanikio ya mkutano wa COP28 utakaofanyika hivi karibuni.
Mabadiliko ya tabianchi ni moja ya changamoto kubwa zaidi zinazoikabili dunia. Mwaka huu, joto ilivunja rekodi ya historia katika majira ya joto, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametahadharisha kuwa, “poromoko la hali ya hewa limeanza”. Bara la Afrika pia limeathiriwa sana na mabadiliko ya tabianchi katika miaka ya hivi karibuni. Baada ya kukumbwa na ukame ambao haujawahi kutokea katika karne moja iliyopita, nchi za Afrika Mashariki zimekumbwa na mafuriko ambayo hayajawahi kutokea katika miaka mia moja iliyopita.
Ushirikiano wa kimataifa ndio chaguo pekee sahihi la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Ikiwa nchi ya kwanza na ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani, na Marekani ikiwa ni nchi kubwa zaidi iliyoendelea na China, ambayo ni nchi kubwa zaidi inayoendelea, ni muhimu sana kwa nchi hizo kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na changamoto hiyo. Ushirikiano kati ya nchi hizo mbili sio tu utahimiza juhudi zao zenyewe, bali pia utaleta msukumo mpya kwa ushirikiano wa jumuiya ya kimataifa. Wakati huo huo, wakati mkutano wa COP28 unakaribia, makubaliano mapya yaliyofikiwa na China na Marekani pia yataleta imani na ujasiri kwa nchi nyingine duniani kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.
China siku zote imetilia maanani ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi. Wakati inahimiza kwa nguvu matumizi ya nishati mpya, na kuboresha muundo wa viwanda ndani ya nchi, pia inatetea ushirikiano wa kimataifa kwa nguvu kubwa. Kwa mfano China dola bilioni 2.75 za Kimarekani kwa Mfuko wa Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kusini, ili kuzisaidia nchi zinazoendelea, zikiwemo nchi za Afrika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.