Tanzania kukamilisha usambazaji wa umeme vijijini ifikapo Juni 2024
2023-11-24 23:43:01| cri

Mamlaka ya usambazaji wa Nishati Vijijini nchini Tanzania (REA) imetangaza kuwa vijiji vyote 12,318 nchini vitapatiwa umeme ifikapo Juni 2024, na kufikia mwisho wa safari iliyoanza miongo mitatu iliyopita. Mafanikio haya itakuwa ni mwaka mmoja kabla ya mpango uliowekwa wa mwaka 2025, wenye lengo la kutoa umeme kwa zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wa vijijini.

Kaimu mkurugenzi wa REA Bw. Johnes Olotu, ameeleza dhamira ya shirika hilo kukamilisha mradi wa usambazaji umeme kabla ya muda uliopangwa, akisema utekelezaji wa mradi huo kwa sasa umefikia wastani wa asilimia 73, na wana imani vijiji vyote vitapata umeme kamili ifikapo mwaka 2024.