Tanzania yatarajia kukamilisha mpango wa usambazaji wa umeme vijijini ifikapo Juni 2024
2023-11-24 08:41:04| cri

Mamlaka nchini Tanzania imesema mpango wa nchi hiyo wa kusambaza umeme katika vijiji vyote 12,318 nchini humo utakamilika ifikapo mwezi wa Juni, mwakani.

Kaimu mkurugenzi wa Mamlaka ya Nishati Vijijini Bw. Johnes Olotu amesema, mpango huo uliopangwa kukamilika mwaka 2025, utatoa umeme kwa zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wa vijijini, na hivyo kuchochea shughuli za kiuchumi.

Bw. Olotu pia amesema, mpango huo ambao umekuwa ukiendelea kwa miongo mitatu sasa, umefikia asilimia 73 ya utekelezaji wake, na kuongeza kuwa, serikali inafadhili mpango huu mkubwa unaogharimu shilingi za Tanzania trilioni 1.58 kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.