Rais wa China ampongeza Bw. Joseph Boakai kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Liberia
2023-11-24 09:51:42| CRI

Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za pongezi kwa Bw. Joseph Boakai kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Liberia.

Katika ujumbe wake rais Xi amesema kutokana na juhudi za Bw. Boakai, sekta zote nchini Liberia zinashikilia kanuni ya kuwepo kwa China Moja, jambo linathaminiwa na China. Amesema watu wa nchi hizo mbili wameshirikiana katika mapambano dhidi ya Ebola na janga la COVID-19, na kufanya ushirikiano wenye ufanisi mkubwa na kujenga urafiki katika maendeleo ya uchumi na jamii. Pia amesisitiza kuwa anatilia maanani sana katika kukuza uhusiano kati ya pande hizo mbili, na kutaka kushirikiana na rais mteule Boakai kukuza urafiki na kuaminiana kati ya nchi hizo mbili, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.