Maonyesho ya uchumi wa bahari ya China ya mwaka 2023 yafunguliwa Shenzhen
2023-11-24 10:00:46| cri

Maonyesho ya uchumi wa bahari ya China ya mwaka 2023 yalifunguliwa jana tarehe 23 mjini Shenzhen, mkoani Guangdong, China. Maonyesho hayo yenye kaulimbiu “uwazi na ushirikiano, ushindi na ushiriki wa pamoja” yamevutia kampuni 658 za sekta husika kutoka nchi na kanda 16, yakifunika eneo la mita za mraba elfu 112.5.

Shughuli za mfululizo zitakazohimiza ubunifu wa teknolojia, maendeleo ya uchumi wa bahari na ushirikiano wa kimataifa zitafanyika kwenye maonyesho hayo huku vifaa, teknolojia, miundo mipya mbalimbali ya uchumi wa bahari vitaonyeshwa.