China yaitaka jamii ya kimataifa iongeze juhudi ili kuhimiza uzinduzi mpya wa Mpango wa Nchi Mbili
2023-11-24 08:41:12| cri


 

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ameitaka jamii ya kimataifa iongeze juhudi ili kuhimiza mustakabali wa siasa wa kuzindua upya Mpango wa Nchi Mbili katika kusuluhisha mgogoro kati ya Israel na Palestina.

Akizungumza jana kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina na Israel Balozi Zhang amesema, mpango wowote wa utatuzi wa hali ya sasa hauwezi kuachana na Mpango wa Nchi Mbili, na lazima usaidie amani na utulivu wa kikanda. Amesema mpango wowote unaohusisha mustakabali wa Palestina lazima ukubaliwe na Wapalestina, na kuzingatia ufuatiliaji wa haki wa nchi za kikanda.

Balozi Zhang pia ameitaka jamii ya kimataifa iongeze juhudi ili kuhimiza kusitishwa kwa mapambano mara moja.