Rais Mwinyi aalika wawekezaji viwanda, biashara kutoka China
2023-11-24 09:44:32| cri

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewakaribisha Zanzibar wafanyabiashara wakubwa na

wenye viwanda kutoka China kuwekeza katika sekta mbalimbali visiwani Zanzibar.

Rais Mwinyi amewakaribishwa wawekezaji hao kwenye mazungumzo yaliyofanyika Novemba 21, Ikulu mjini Unguja alipokuwa akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye viwanda na wafanyabiashara 15 kutoka China, Bw. Xu Lejiang. Amewaeleza kuwa utalii hasa wa hoteli na maeneo ya kupumzikia una fursa nyingi za uwekezaji, kwani Zanzibar ina maeneo mazuri ya fukwe nyeupe zinazowavutia wageni na watalii wengi.

Bw. Xu Lejiang amemweleza Dk Mwinyi kwamba shirikisho hilo limeziweka pamoja zaidi ya kampuni kubwa na viwanda 700 wakiwemo wafanyabiashara wa madini, kampuni za vifaa vya ujenzi, teknolojia na kilimo.