MONUSCO watangaza kuondoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
2023-11-24 09:59:05| cri

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(MONUSCO)umesema tarehe 22 kuwa utaondoka nchini humo kufuata utaratibu na kwa njia inayowajibika.

Hivi karibuni ujumbe huo ulisaini makubaliano ya kuondoka kutoka DRC na serikali ya nchi hiyo yakisema uondokaji wao utatekelezwa kwa vipindi vitatu, lakini ratiba na mpango halisi bado havijatangazwa.

MONUSCO imekuwepo kwenye eneo la mashariki la DRC tangu mwaka 1999. Tarehe 30 mwezi huu, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litajadili kurefusha muda wa uwepo wa ujumbe huo nchini humo, na ujumbe huo unakadiriwa kuondoka hatua kwa hatua baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kufanyika tarehe 20 mwezi ujao.