Rwanda yapongezwa kwa kuendeleza haki za ardhi za wanawake
2023-11-25 23:43:33| cri

Juhudi za Rwanda katika kuendeleza haki za ardhi za wanawake zimepongezwa na maofisa katika sehemu ya tano inayoendelea ya Mkutano wa Sera ya Ardhi Barani Afrika (CLPA), ulioanza Novemba 21 na kumalizika leo mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Mbali na Rwanda, Kenya na Tanzania pia zimepongezwa shirika la kimataifa la haki za ardhi na hisani la wanawake (LANDESA) kwa juhudi zao za kupigania haki ya ardhi ya wanawake kupitia kampeni za ubunifu za uhamasishaji, ikiwa ni pamoja na matumizi ya vitabu vya sauti ili kuwaelimisha wanawake wasiojua kusoma na kuandika na wasio na uwezo.

CLPA, mkutano unaofanyika mara mbili kila mwaka unaoitishwa na Kituo cha Sera ya Ardhi Afrika (ALPC), unatoa jukwaa muhimu kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kujadili masuala muhimu yanayohusiana na ardhi na kuandaa mapendekezo yanayotekelezeka.