Xi aongoza mkutano kuhusu maendeleo ya ukanda wa kiuchumi wa Mto Yangtze na uongozi wa CPC juu ya mambo ya nje
2023-11-27 15:25:44| cri

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) leo imefanya mkutano wa kupitia ripoti ya sera na hatua za kukuza zaidi maendeleo ya hali ya juu ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Yangtze.

Katibu mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China, Xi Jinping, aliongoza mkutano huo, ambao pia ulijadili miongozo mbalimbali ya uongozi wa CPC kuhusu mambo ya nje.