Waziri wa mambo ya nje wa China ahimiza China, Japan na Korea Kusini kutoa mchango zaidi kuhimiza maendeleo ya kikanda na kimataifa
2023-11-27 08:41:51| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi amesema China, Japan na Korea Kusini zinapaswa kuchukua jukumu kubwa zaidi katika kuhimiza maendeleo ya kikanda na kimataifa, yanayokabiliwa na mabadiliko ya kasi ambayo hayajaonekana katika miaka mia moja iliyopita na kufufuka polepole kwa uchumi wa dunia. 

Bwana Wang amesema hayo mjini Busan kwenye mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China, Japan na Korea Kusini.

Bw. Wang amesema ushirikiano kati ya China na Japan na Korea Kusini umekuwa utaratibu wa ushirikiano wa pande nyingi wa ngazi ya juu, unaochukua eneo kubwa sana na maana ya kina katika eneo la Asia Mashariki, ambao umesaidia ipasavyo maendeleo ya nchi hizo tatu na kuwanufaisha watu wa nchi hizo na wa kanda nzima ya Asia Mashariki.