​ Somalia yaimarisha hatua za kukabiliana na mafuriko
2023-11-27 08:56:11| CRI

Serikali ya Somalia na mashirika ya kibinadamu wameimarisha hatua za kukabiliana na maafa ikiwemo operesheni za uokoaji katika maeneo yanayoathiriwa na mafuriko wakati idadi ya vifo kutokana na mvua kubwa na mafuriko vilivyosababishwa na El Nino ikiongezeka hadi kufikia karibu 100.

Idara ya usimamizi wa maafa ya Somalia imesema, watu zaidi ya 96 wamefariki kutokana na mafuriko makubwa yaliyoathiri watu wengine milioni 2.3 nchini humo.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa mafuriko hayo yamezidisha msukosuko wa njaa nchini Somalia huku watu milioni 4.3 wakikadiriwa kukabiliwa na njaa kali hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Mafuriko hayo pia yameharibu miundombinu na kuathiri biashara, elimu na huduma za utoaji wa chakula kote nchini.