Israel na kundi la Hamas waachia huru kikundi cha tatu cha watu wanaoshikiliwa
2023-11-27 08:34:21| CRI

Kikosi cha Qassam cha kundi la Hamas kilitoa taarifa jana Jumapili kikitangaza kuwaachia huru kikundi cha tatu cha watu wanaowashikilia, wakiwemo waisraeli 13, raia watatu wa Thailand na mmoja wa Russia. Habari kutoka Shirika la Habari la Palestina zinasema, Israel siku hiyo iliwaachia vijana 39 wa Palestina.

Taarifa iliyotolewa jana na Kundi la Hamas inasema kundi hilo linatafakari kuwaachia huru watu wengi zaidi wanaoshikiliwa ili kubadilishana na muda zaidi wa usitishwaji vita kwenye ukanda wa Gaza.

Kabla ya hapo, kundi la Hamas limewaachia huru vikundi viwili vya watu 41 waliowashikilia, na upande wa Israel pia umewaachia vikundi viwili vya wapalestina 78, tangu usitishwaji vita wa siku nne uanze kutekelezwa Novemba 24.