Mtu mmoja auawa katika shambulizi kaunti ya Lamu, Kenya
2023-11-27 08:59:33| CRI

Mtu mmoja ameuawa na nyumba kadhaa zilichomwa moto katika shambulizi lililotokea Jumamosi dhidi ya vijiji viwili vya kaunti ya Lamu nchini Kenya.

Kamishna wa kaunti hiyo Bw. Louis Rono amesema washambulizi waliobeba silaha walivamia vijiji vya Marafa na Poromoko saa tatu hivi usiku wa Jumamosi iliyopita. Sasa polisi wameanza kuwasaka washambulizi hao.

Shambulizi hilo linalodhaniwa kufanywa na wapiganaji wa kundi la al-Shabab, limekuja miezi mitatu tu baada ya shambulizi lingine lililofanana hilo kutokea huko Lamu Magharibi. Polisi wamesema wameimarisha operesheni za usalama katika eneo hilo ili kuzuia mipango mingine ya mashambulizi.