Dereva wa Uganda ashinda Ubingwa wa Kitaifa wa Mbio za Magari Tanzania
2023-11-27 22:56:23| cri

Chama cha Magari Tanzania (AAT) kimesema kuwa Dereva wa Uganda Yassin Nasser ameshinda Ubingwa wa Kitaifa wa Mbio za Magari za Kitaifa (NRC).

Kwa mujibu wa ripoti ya mwisho iliyotolewa na mkurugenzi wa mbio hizo wa Chama cha Magari Tanzania (AAT) Satinder Birdi, Nasser amejikusanyia pointi 94 kutokana na matukio matatu.

Ripoti hiyo inaonesha kuwa Nasser alijinyakulia pointi 30 katika mashindano ya Iringa Motorsport kabla ya kutwaa pointi nyingine 30 kutoka kwenye mashindano ya Mlima Usambara na baadaye kufikisha pointi 34 kutokana na mchezo uliomalizika hivi punde wa AAT uliofanyika mkoani Iringa.

Katika mbio hizo Randeep Birdi alishika nafasi ya pili akiwa na pointi 84. Birdi alikusanya pointi 24 katika mashindano ya Mlima Usambara Motorsport na baadaye akapata pointi 60 katika mashindano yaliyomalizika hivi punde ya AAT. Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Manveer Bird mwenye pointi 84 na Gurpal Sandhu wa Arusha alishika nafasi ya nne akiwa na pointi 72. Dereva aliyemaliza katika nafasi ya tano bora ni Kelvin Taylor aliyekusanya pointi 43.