Pembe 24 za tembo zanaswa katika operesheni ya siri nchini Namibia
2023-11-27 09:03:46| CRI

Mamlaka ya Namibia imekamata pembe 24 za tembo katika operesheni iliyoongozwa na wizara ya mazingira, misitu na utalii na maofisa wa usalama, ikilenga kundi la Zambia linalojihusisha na ujangili wa tembo wa kimataifa nchini Botswana kupitia mkoa wa Zambezi.

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili, msemaji wa wizara hiyo Bw. Romeo Muyunda alisema maofisa wa usalama walizuia gari lililotumiwa kusafirisha meno ya tembo lakini walifanikiwa kumkamata mshukiwa mmoja tu, na wengine saba walitoroka.

Bw. Muyunda amepongeza hatua ya haraka ya idara ya utekelezaji wa sheria, akisisitiza kujitolea kwa Namibia katika kupambana na uhalifu wa wanyamapori.