Kenya yaimarisha mwitikio dhidi ya mafuriko wakati idadi ya vifo inaongezeka hadi 76
2023-11-28 09:04:50| CRI

Baraza la mawaziri la Kenya jana Jumatatu limeazimia kuimarisha hatua za mwitikio dhidi ya mafuriko nchini kote wakati idadi ya vifo vilivyosababishwa na mafuriko hayo ikiongezeka hadi 76.

Baraza hilo lilifanya mkutano wa dharura ulioongozwa na Rais William Ruto mjini Nairobi na kuagiza kutenga shilingi nyingine bilioni 10 (takriban dola za kimarekani milioni 65.5) kwa serikali za kaunti kuimarisha hatua za kupunguza athari za El Nino.

Habari zinasema mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua kubwa za El-Nino yamesababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao, Baraza hilo limesema kaunti 38 kati ya zote 47 ziko katika hali ya tahadhari, kutokana na hatari ya kutokea kwa mafuriko ya ghafla na maporomoko ya ardhi yanayoweza kudhuru mifugo na mashamba.