Xi asisitiza maendeleo ya mfumo wa sheria unaohusiana na mambo ya nje
2023-11-28 15:34:54| cri

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza haja ya kuimarisha mfumo wa sheria unaohusiana na mambo ya nje.

Rais Xi ameyasisitiza hayo wakati akiongoza darasa la mafunzo la Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC jana Jumatatu. Ametilia mkazo haja ya kuunda mazingira ya utawala unaozingatia sheria na mazingira mazuri ya nje kwa ajili ya kuendeleza China ya kisasa.

Xi alirejea tena kwamba kuimarisha utawala wa sheria katika mambo ya nje kunatumikia mahitaji ya muda mrefu ya kujenga taifa lenye nguvu na kuendeleza ufufuaji wa taifa kupitia njia ya China ya kisasa. Aidha alisisitiza zaidi umuhimu wa haraka wa maendeleo ya mfumo wa kisheria unaohusiana na mambo ya kigeni katika kukuza ufunguaji mlango wa hali ya juu na kushughulikia hatari na changamoto za nje.

Akitoa wito wa kuzingatiwa umuhimu na udharura wa suala hilo, Xi alisisitiza haja ya kustawisha mfumo wa kisheria unaohusiana na nchi za nje na uwezo unaokidhi mahitaji ya maendeleo ya hali ya juu na ufunguaji mlango wa hali ya juu.

Profesa katika Chuo Kikuu cha Wuhan alitoa hotuba, baada ya hapo wajumbe wa Ofisi ya Kisiasa walifanya majadiliano.