Baraza la amani na urafiki la Basi la mwaka 2023 lafanyika
2023-11-28 20:04:04| CRI

Baraza la amani na urafiki la Basi la mwaka 2023 limefanyika leo tarehe 28 Novemba katika mji wa Dujiangyan, mkoani Sichuan. Baraza hilo limeandaliwa kwa pamoja na shirikisho la mawasiliano ya kirafiki ya kimataifa la China na Shirika Kuu la utangazaji la China CMG.

Baraza hilo lenye kauli mbiu ya “Kufanya Mawasiliano ya kirafiki, Kunufaisha amani”, limehudhuriwa na wajumbe kutoka Marekani, Italia, Ubelgiji, Qatar, Morocco, Sri Lanka na nchi nyingine.

Basi ni jina la panda aliyeishi kwa miaka mingi zaidi duniani, alifariki dunia mwezi Septemba mwaka 2017. Alialikwa kufanya ziara nchini Marekani mwaka 1987, alikuwa “balozi" wa amani wa mawasiliano kati ya watu wa China na nchi za nje. Baraza hilo linatoa masimulizi ya ajabu ya “Basi” kwa jumuiya ya kimataifa, na kutumia fursa hii kufafanua kwa pande mbalimbali fikra ya Xi Jinping kuhusu ustaarabu wa kiikolojia, kuhimiza ulinzi wa mazingira ya asili ya sayari ya dunia, kulinda anuai ya baiolojia, na kujitahidi kujenga jumuiya ya pamoja kati ya binadamu na maumbile.