IGAD yaandaa mkutano nchini Kenya kujadili suala la watu waliolazimishwa kukimbia makazi
2023-11-28 08:56:23| CRI

Mamlaka ya maendeleo ya kiserikali ya Afrika Mashariki IGAD imeitisha mkutano wa ngazi ya juu wa kikanda mjini Nairobi kuhusu watu waliolazimika kukimbia makazi yao.

Mkutano huo wa siku mbili uliohudhuriwa na nchi wanachama wa IGAD, wadau wa maendeleo, mashirika ya Umoja wa Mataifa, sekta binafsi, wakimbizi na jamii za kiraia unalenga kuendeleza hatua za kukabiliana na suala la watu waliolazimika kukimbia makazi yao katika kanda hiyo.

Mohamed Elduma, mkuu wa kitengo cha maendeleo ya kijamii katika Idara ya Maendeleo ya afya na jamii ya IGAD amesema, mkutano huo utasaidia kubadilisha hali ya wakimbizi katika kanda hiyo, huku akiongeza kuwa wanatarajia kuendeleza mtindo wa kukabiliana na wakimbizi kutoka njia ya matunzo na kibinadamu ili kuwawezesha pamoja na jamii zinazowapokea.