Kenya yazindua mpango wa miaka 10 wa kukuza uchumi wa kidijitali
2023-11-28 08:53:02| CRI

Rais William Ruto wa Kenya amezindua mpango wa miaka kumi wa kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali kupitia kuwekeza katika mfumo thabiti wa uvumbuzi, mafunzo, ushauri na uhusiano wa soko.

Mpango huo umezinduliwa pembeni mwa Wiki ya tatu ya uvumbuzi ya Kenya inayoendelea mjini Nairobi, yenye lengo la kuhimiza uwepo wa miundombinu wezeshi, mafunzo, na upatikanaji wa mitaji kama njia ya kuharakisha ukuaji wa uanzishaji wa teknolojia nchini Kenya.

Rais Ruto amesisitiza dhamira ya Kenya ya kuwa kituo cha uvumbuzi cha kikanda, akiongeza kuwa wawekezaji na wajasiriamali wana nia ya kuingiza mtaji kwenye kuanzisha biashara za ndani, zinazohimiza matumizi ya teknolojia za kidigitali kwenye sekta binafsi na ya umma.