Ujenzi wa kiwanda cha saruji kinachojengwa na kampuni ya China nchini Ethiopia wafikia asilimia 70
2023-11-28 08:53:40| CRI

Ujenzi wa Kiwanda cha Saruji cha Lemi nchini Ethiopia unaotekelezwa na kampuni ya China, umekamilika kwa asilimia 70 na kiwanda hicho kinatazamiwa kuzinduliwa mapema mwaka kesho na kuongeza uwezo wa uzalishaji wa saruji wa Ethiopia kwa tani za ujazo milioni 8.

Kiwanda hicho kinajengwa kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 600 kaskazini mwa Addis Ababa.

Miundo muhimu ya kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na ile ya kuyeyusha miamba kwa joto kali tayari imekamilika, ambayo ni hatua muhimu ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi ya Sinoma inayotekeleza ujenzi huo Bw. Lin Zhong, amesema Kiwanda cha saruji cha Lemi kinatarajiwa kukamilika Machi 2024.