Mkoa wa Shaanxi wa China na Dar es Salaam kutafuta ushirikiano wa siku za baadaye
2023-11-28 08:57:09| CRI

Mkoa wa Shaanxi wa China na mkoa wa Dar es Salaam wa Tanzania wamesaini makubaliano yanayolenga kutafuta fursa za uwekezaji na kuunga mkono maendeleo ya kiuchumi kwa pande zote mbili.

Makubaliano hayo ambayo ni waraka wa kulenga kuendeleza mikoa rafiki kati ya Shaanxi na Dar es Salaam yamesainiwa kati ya Li Mingyuan, mjumbe wa kamati ya kudumu ya Chama cha Kikomunisti cha China ya mkoa wa Shaanxi na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Albert Chalamila.

Bw. Chalamila amesema makubaliano hayo yatawawezesha wawekezaji kutoka mkoa wa Shaanxi na Dar es Salaam kutafuta fursa za uwekezaji zinazopatikana jijini Dar es Salaam.

Balozi wa China nchini Tanzania Bibi Chen Mingjian, amesema mkoa wa Shaanxi una miji ya kisasa pamoja na raslimali za elimu na viwanda, huku Dar es Salaam ikiwa kituo cha biashara na uchukuzi kinachohudumia nchi nane zisizo na bahari, na ina uwezo mkubwa wa kubadilishana na kushirikiana katika sekta mbalimbali.