Jeshi la Sudan latangaza kufanya operesheni ya ardhini ili “kuwatokomeza” RSF
2023-11-29 14:43:08| cri

Jeshi la Sudan (SAF) Jumanne lilitangaza kuanzisha operesheni ya ardhini likielekea mji mkuu wa Sudan, ili “kutokomeza” Vikosi vya msaada wa haraka (RSF).

Kamanda mkuu msaidizi wa SAF Yasir Al-Atta aliwaambia askari na maofisa wa eneo la kijeshi la Omdurman kuwa, jeshi limeanza kampeni, maeneo yote ya kijeshi yako tayari, na watakwenda pande zote.

Al-Atta alipongeza juhudi na uungaji mkono wa watu wa Sudan kwa jeshi lake katika kulinda taifa la Sudan na kushinda RSF, huku akishutumu baadhi ya nchi na mashirika ya kimataifa na ya kikanda kwa kuiunga mkono RSF.