Watalii 30 wageni wako salama baada ya ndege yao kutua vibaya katika mbuga ya wanyama mashariki mwa Tanzania
2023-11-29 08:59:10| CRI

Watalii wote 30, marubani wawili na mhudumu mmoja wako  salama baada ya ndege yao kutua vibaya katika uwanja uliopo kwenye mbuga ya wanyama ya Mikumi iliyoko mashariki mwa Tanzania.

Ofisa habari wa Mamlaka ya hifadhi na Mbuga za Wanyamapori za Tanzania TANAPA Bi Catherine Mbena ametoa taarifa ikisema, ndege hiyo ya aina ya Embraer EMB 120 Brasilia iliyoruka kutoka Zanzibar, ilikumbwa na mkasa huo baada ya kukumbwa na tatizo la kiufundi.

Taarifa imesema marubani walifanya juhudi kwa kushirikiana na maofisa wa uwanja kuhakikisha usalama wa abiria wote, na kuongeza kuwa watalii waliendelea na mpango wao wa kutalii katika mbuga hiyo.