Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC ahitimisha uchunguzi wa ghasia za uchaguzi wa 2007 nchini Kenya
2023-11-29 23:39:01| cri

Naibu Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Nazhat Shameen Khan Jumatatu alitangaza kwamba anafuta uchunguzi zaidi kuhusu uhalifu uliofanyika nchini Kenya kuhusiana na ghasia zilizozuka kufuatia uchaguzi wa mwaka 2007.

Uamuzi huo unahitimisha sakata la kisheria lililoendelea kwa miaka 13 ambalo liliwahusisha wanasiasa wakuu wa Kenya. Kwenye taarifa yake Nazhat Shameen Khan alisema amefikia uamuzi huu baada ya kuzingatia ukweli maalum na mazingira ya hali hii.

Sambamba na hilo, amesema Ofisi haitafuatilia kesi za ziada katika madai ya jinai ya watu wengine.

Mwaka 2010, mahakama hiyo yenye makao yake mjini The Hague ilianza kuchunguza mapigano baada ya uchaguzi katika taifa hilo ambapo waendesha mashtaka walisema watu 1,300 walikufa na wengine 600,000 waliachwa bila makazi.