Xi Jinping afanya ziara ya ukaguzi mjini Shanghai 
2023-11-29 21:56:27| cri

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Xi Jinping alifanya ziara ya ukaguzi katika mji wa Shanghai mashariki mwa China kuanzia Jumanne hadi Jumatano.

Katika safari yake hiyo, Xi alikagua Soko la kununuliwa na kuuzwa kwa hatima za bidhaa (Shanghai Futures Exchange), maonyesho ya uvumbuzi wa teknolojia ya sayansi ya Shanghai, na jumuiya ya nyumba za kupangisha zinazofadhiliwa na serikali, akifahamishwa kuhusu jitihada za mji huo katika kuimarisha ushindani wake kama kituo cha fedha cha kimataifa, kujenga mji huo kuwa kituo cha uvumbuzi wa teknolojia ya sayansi cha kimataifa na kujenga miradi ya nyumba za kupangisha zinazofadhiliwa na serikali.