Rais Xi aongoza mkutano kuhusu maendeleo ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang, na uongozi wa CPC kuhusu mambo ya nje
2023-11-29 09:04:24| CRI

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) tarehe 27 Novemba ilifanya mkutano wa kupitia Miongozo ya Sera na Hatua za Kuhimiza Zaidi Maendeleo ya Hali ya Juu ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang, na Kanuni za Uongozi wa Chama kuhusu Mambo ya Nje, chini ya uenyekiti wa Rais Xi Jinping.

Kwenye mkutano huo, imebainika kuwa mkakati wa maendeleo ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang ni uamuzi mkubwa wa kimkakati uliofanywa na kamati kuu ya chama na Komredi Xi Jinping akiwa kiini chake.

Tangu mkakati huo uanze kutekelezwa, mabadiliko makubwa yametokea katika uelewa wa mkakati, mazingira ya ikolojia, mtindo wa maendeleo, ushirikiano wa kikanda, na mageuzi na ufunguaji mlango, na matokeo yake yamekuwa ni kuongezeka kwa kasi kwa ubora wa maendeleo, na hali inazidi kuwa nzuri.

Imefahamika pia kwenye mkutano huo kuwa kanuni za Chama cha Kikomunisti cha China kwenye uongozi wa mambo ya nje, zimeleta mageuzi kwenye miongozo ya chama, na kuwa na mchango mkubwa kwenye mifumo iliyofanyiwa majaribio na uzoefu uliopatikana, ambayo imekuwa muhimu katika utekelezaji wa sera, kanuni na mipango mkakati inayotolewa na kamati kuu ya chama kuhusu mambo ya nje.