Wanajeshi wa Somalia wawaua wanamgambo 6 wa kundi la al-Shabaab katika eneo la kati
2023-11-29 08:52:58| CRI

Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) likisaidiwa na vikosi vya ndani jana liliwaua wanamgambo sita wa kundi la al-Shaabab na kuwajeruhi wengine katika operesheni jimboni Galmudug, katikati mwa Somalia.

Naibu waziri wa habari, utamaduni na utalii wa Somalia Bw. Abdirahman Yusuf Al-Adala amesema vikosi vya pamoja pia vilifanikiwa kukamata silaha katika operesheni hiyo.

Jeshi la SNA na wenyeji walifanya operesheni zilizofanikiwa dhidi ya magaidi mashariki mwa eneo la Galgaduud usiku kucha, vikosi hivyo bado vinawasaka wanamgambo waliotoroka wakati wa operesheni, na jeshi limedhibiti kikamilifu eneo hilo.