Serikali ya Sierra Leone yayataja mashambulizi ya Jumapili kuwa ni “jaribio la mapinduzi”
2023-11-29 08:19:53| CRI

Serikali ya Sierra Leone imesema mashambulizi yaliyofanywa Jumapili na watu wenye silaha dhidi ya kambi ya kijeshi, gereza na maeneo mengine mjini Freetown, ni “jaribio la mapinduzi lililoshindwa”.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari na Elimu ya Umma Chernor Bah kwenye mkutano na wanahabari, akisema watu 14, wakiwemo wanajeshi 12 na raia mmoja wa kawaida, wamekamatwa, na wanawasaidia Polisi kwenye uchunguzi.

Polisi wanawasaka wafungwa waliotoroka kwenye tukio hilo, ambao baadhi yao wamejisalimisha kwa mamlaka ya gereza.