Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha yamesababisha vifo vya watu wanane wakiwemo watoto watatu katika mkoa wa Tanga, kaskazini mwa Tanzania.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi, amesema, mafuriko hayo yamesababisha vifo vya watu katika wilaya za Tanga, Muheza na Handeni katika wiki tatu zilizopita.
Kamanda Mchunguzi pia ameongeza kuwa mvua kubwa imeharibu miundombinu ya mkoa huo hasa barabara na madaraja.